Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa


Wengi wetu tumekuwa ni watumiaji wazuri wa
simu zetu pengine hata kufikia kulala nazo
kitandani ama tukitaka tusipitwe na simu
fulani ya muhimu ama kwa sababu tunapitiwa
na usingizi wakati bado tunachati.
Tabia hii sio salama kwa afya na usalama
wetu, makala hii itakusaidia kuelewa madhara
yaliyopo iwapo unalala na simu yako ikiwa
imewashwa.
Jambo la kwanza ni kwamba simu kama kifaa
cha kielektroniki inaweza kusababisha shoti ya
umeme muda wowote hasa ikiwa inachajiwa,
hili linzweza kusambabisha madhara mengi
ikiwamo lile la moto. Pia kwa bahati mbaya
wengi wetu huwa hatusomi maelezo ya jinsi
ya kutumia simu zetu na mara nyingi kuna
matumizi ya chaja zisizokuwa rasmi na
zilizochini ya ubora…na muda mwingine ata
betri za simu zinazonunuliwa muda wa
kubadilisha zinakuwa zilizochini ya kiwango.
Kulala na simu ni Hatari : Simu janja ikiwa
imeungua baada ya kuwekwa chini ya mto .
Picha kwa hisani ya mtandao
Jambo la pili ni kwamba kwa kutumia simu
kitandani kuna uwezekano mkubwa sana
ukaharibu mfumo wako wa usingizi, ingawa
wengi wetu hatujali sana hili lakini ni kweli
kwamba ufanisi wako wakati wa mchana
unategemea hasa ulilalaje wakati wa usiku.
Mwanga unaotokana na simu yako unasifika
kwa kubadili namna ambayo wewe ulikuwa
unalala na mwanga huu hukufanya usilale na
kupumzika vizuri.
Inaaminika kwamba simu zinatoa mionzi
ambayo inaweza kusababisha kansa, ingawa hili
bado limewagawanywa watafiti lakini hata
shirika la afya duniani limeisha waonya watu
dhidi ya madhara hayo ambayo bado
yanachunguzwa. Watafiti bado wanaendelea
kufanya uchunguzi ila kuna tafiti mbalimbali
zinakuja na matokeo tofauti – wengine
wakisema hakuna uhusiano kati ya utumiaji
simu na kansa huku wengine wakisema
uhusiano upo ila ni mdogo na madhara ya
utumiaji yanatokea miaka mingi sana baadae.
Hapa tunakuachia wewe – ila ushauri mzuri ni
BORA KINGA… – Vyanzo NYDailyNews, na
Cancer.Gov
"ushauri "  Hivyo basi kisayansi unashauriwa kuwa ni bora/nafuu kutumia earphones kusikiliza simu ambazo zinazidi dakika ishirini na kama una mtoto mdogo usiruhusu kabisa asikilize simu wala kuchezea simu maana fuvu la kichwa chake bado ni changa hivyo ni rahisi zaidi kwake kuathirika ukilinganisha na watu wazima.
Share on Google Plus

About mboo safi nene na ndefu

0 comments:

Post a Comment