MAMBO MUHIMU AMBAYO SIKU ZOTE YANASABABISHA KUHARIBU “HARDWARE” KWENYE KOMPYUTA YAKO.
Tunapozungumzia “Hardware” hapa tuna maana ya vitu ambavyo vinaweza kugusika n ahata kuviona kwa macho kwenye Kompyuta yako. Hapa tuna maana ya vitu kama Battery, Motherboard, kioo, keyboard, n.k.
Kompyuta kama kilivyo kitu chochote kina mwisho wa kuishi, na pia kila kitu kinahitaji matunzo ili kiweze kuishi kwa Muda mrefu. Matunzo hayo yanahusu Kompyuta mpya au hata ambayo imeishatumika.
Katika matumizi yako ya Kompyuta unatakiwa kujua mambo haya kuwa uonapo tatizo lolote yawezekana limetokea jambo hilo;
1.Kuwepo kwa Uchafu kwenye Kompyuta yako. (Dust build up)
Hapa hutokea pale ambapo unakuta uchafu unajikusanya sehemu moja wapo kwenye Kompyuta na kutengeneza mafungu mafungu ambapo mwishowe huathiri Kompyuta na kusababisha kuwepo kwa joto jingi maana feni inashindwa kufanya kazi kwa ufasaha. Hivyo unatakiwa kuwa na mazoea ya kufungua Kompyuta yako na kuisafisha ili kuondoa uchafu huo.
2.Kutokuwepo kwa hewa ya kutosha kwenye Kompyuta. (Poor ventilation).
Kwa kawaida Kompyuta nayo huitaji hewa ya kutosha ili kuweza kupumua kwa umakini wa hali ya juu, uwepo wa hali nzuri ya hewa husababisha kuwepo kwa ubaridi unaosababisha kupoza baadhi ya vifaa kwenye Kompyuta hasa pale vinapopata joto sana. Tatizo hili mara zote hutokana na Feni kutofanya kazi vyema. Joto jingi kwenye Kompyuta huweza kusababisha matatizo mengi sana. Matokeo yake ni Kompyuta kuwa nzito, kupiga kelele na hata kuonesha kushindwa kufanya kazi kabisa.
3.Kupoteana au kukatika kwa kebo/ nyaya.
Cable/nyaya kwenye Kompyuta zinatakiwa kukaa kwenye mfumo ambao unafanana na unaoendana kwa utaratibu muhimu sana, hapa nazungumzia kuwa Kebo zinatakiwa kwenda kwa utaratibu maalumu maana bila kufanya hivyo na kuchanganyana inaweza kusababisha hata “short” kwenye Kompyuta yako.
4. Kutumia “charger”/ “Adapter” ambayo sio model yake.
Watumiaji wa baadhi ya Kompyuta wameshindwa kujua kuwa Adapter haziingiliani katika kucharge kumpyuta yako, mfano utakuta mtu anatumia Adapter ya Dell kucharge HP Kompyuta na mwingine anatumia Adapter yenye uwezo mdogo au mkubwa ziadi ya Kompyuta yake, kitendo kinachoweza kusababisha “Short|” kwenye Kompyuta yako.
5. Kutokutunza betri ya Kompyuta.
Hakikisha betri lako linatunzwa katika hali ya umakini sana, pia unapokuwa unanunua Betri la Kompyuta yako, hakikisha liendane na Kompyuta yako. Na wakati wa Kutumia Kompyuta yako, hakikisha umecharge mpaka limeonesha 100% na baada ya hapo ondoa “Chager” yako, endelea kutumia mpaka pale itakoonesha kuhitaji kuchaji tena, hii itakusaidia kutunza betri lako n ahata kuondoa uwezekano wa kutokea tatizo jingine kwenye Kompyuta yako.
6. Kuangusha/ kupata ajali kwa Kompyuta yako.
Wakati mwingine pale inapotokea ajali ya kuangusha Kompyuta inaweza kusababisha kuvunjika/kuharibika kwa vitu mbalimbali vinavyounda mfumo mzima wa Kompyuta. Pale Kompyuta inapoanguka inaweza kutokea kuharibika kwa kioo, kuvunjika kwa bawaba, na hata kuharibika kwa vitu vingine kwenye Kompyuta.
7. Kumwagiwa kimiminika Kompyuta.
Tumekuwa tukisistiza pale unapokuwa unatumia kimiminika kama soda, chai, uji, maji n.k uwe makini sana maana kikimwagika kwenye kompyuyta yako hasa kwenye Keyboard, kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha kuharibika kwa Kompyuta yako kwa ujumla na matokeo yake san asana huwa ni kuzima kwa Kompyuta yako.
8.Kusasisha (update) software,
Pale unapokuwa unatumia Kompyuta zipo software ambazo hutumika kwa ajili ya kuendesha mfumo wa utendaji wa Kompyuta, lakini pia zinatakiwa ziwe zina sasisha(update) kutokana na matumizi yako kwa ujumla. Pia napenda kukuambia kuwa sio kila software inafaa kwa matumizi ya Kompyuta yako, maana baadhi ya software zinaweza kusababisha hata Kompyuta yako kuzima na isiweze kufanya kazi kabisa.
Suluhisho la matatizo yote kwenye mfumo mzima wa Kompyuta yako ni kuwa na mazoea yafanya “SERVICE” au kuwa na “Technician” aliyebobea kwenye suala zima la Matengenezo ya Kompyuta pande zote kwenye “Hardware” na “software”.
Share with your friend
0717692952
0 comments:
Post a Comment