HII NDIO SAMSUNG S3

Samsung Waleta Galaxy S III Mini!

Baada ya kampuni ya Samsung kufanya vizuri kimauzo kupitia simu yake maarufu ya Samsung Galaxy S III kampuni hiyo imeamua kutoa toleo dogo la simu hiyo linalotambulika kama 'Galaxy S III Mini'.




Samsung Galaxy S III imefanya vizuri sana sokoni na kuwa moja ya simu za kisasa iliyouzika zaidi na inaendelea kuuzika hadi sasa. Wazo la kutoa toleo dogo la simu hiyo wengi wanachukulia kama hatua ya kuongeza ushindani zaidi dhidi ya iPhone 5, na watafiti wengi wa soko la simu wanaona Samsung wamefanya uamuzi mzuri katika hili.

Samsung Galaxy S III inakioo kikubwa sana, na pia ghari sana ikiuzika kwa bei ya zaidi ya laki tisa, hivyo kuleta toleo hili la 'Mini' wanategemea kuvutia watu wasiopenda vioo vikubwa sana na pia kuvutia soko kubwa zaidi kwa bei ya chini.

Toleo Mini Na Kubwa

  • 1GHz dual-core processor,
  • 1GB RAM, 
  • Kioo/Display cha inchi 4 (Galaxy SIII kubwa inakioo cha inchi 4.8)
  • WVGA AMOLED screen
  • Hadi ukubwa wa GB 16
Inategemewa bei ya Samsung Galaxy S III mini itakuwa kwenye laki sita hadi saba, na imeshaingizwa sokoni kwenye baadhi ya nchi barani ulaya.

Share on Google Plus

About mboo safi nene na ndefu

0 comments:

Post a Comment