GRAPHICS DESIGNING NI NINI? NI KIPI MUHIMU KUKIJUA KATIKA GRAPHICS ILI KUWEZA KUWA MSHINDANI MZURI KATIKA KU DESIGN ? TWENDE PAMOJA HAPA UTAELEWA TU

Image result for graphics designGraphic Designing ni elimu inayotolewa kwa mtu kwa mafunzo ya kuchora, kuandika, kupamba, ketengeneza picha mbalimbali kwa ujuzi wa computer. Ujuzi huu hutumia msaada wa program maalum ambazo hutumika katika kufanya graphic designing. 
    Michoro yenye mapambo, matangazo, maandishi yanayovutia na picha mbalimbali unazoziona ndani na nje ya internet ni matokeo ya kazi hii ya graphic designing. Kazi hii imekuwa ni bora kwa ulimwengu wa sasa wa kiteknolojia kwani watu huhitaji sana vijana wenye ujuzi wa hii, kuwatengenezea matangazo, michoro na mambo mengi ya kuvutia katika kutangaza biashara zao.
     Hata wale wanaotengeneza kadi za harusi au za mchango na nyinginezo hutumia ujuzi huu.     Kwa wale ambao ndio wanaanza kujifunza hutumia sana Microsoft Office Publisher kwani ndio program rahisi na haina mambo mengi ya kuchanganya na hata kuisomea hii katika vyuo inakuwa na gharama ndogo ukilinganisha na nyinginezo. Mara nyingi wanaotengeneza kadi mbali mbali kama vile za harusi, mualiko, mchango, vitambulisho vidogo hupenda sana kutumia Microsoft Office Publisher.

Image result for photoshop cs6
     Kwa sasa program kubwa sana inayotumika ulimwenguni katika kufanya graphics ni Adobe Photoshop na Adobe illustrator lakini kuna tofauti sana hapo, Adobe Photoshop ni nzuri sana  kwaajili ya kuhariri (edit) picha, au kutengeneza mabango ya matangazo ya sanaa kama vile wasanii, muziki n.k. ndio utaona mtu amepiga picha chumbani lakini kwa kutumia Photoshop amewekwa bafuni. Au mtu anapiga picha porini halafu anatumia photoshop kujiweka katikati ya miji mikubwa duniani. Illustrator ni nzuri kwa wanaotengeneza michoro wenyewe upya, unaweza kutumia program hii kuchorea, kutengeneza vitu mbalimbali vyenye kuvutia kama vile mandhari, pia unaweza kutumia hii kutengeneza Business cards, post cards, CD/DVD covers na mengi katika hayo. Lakini kumbuka kuwa kila mtaalamu anaweza akatumia program anayoona kwake ni rahisi, na zote hizo zinaingiliana ni wewe tu na ujuzi wako.

     Na program za kufanya graphics zenye kujongea (motion graphics) ni kama vile Adobe Flash, Adobe After Effect. Ila Adobe Flash ni kwa graphics za ndani ya website, ndio maana utaona picha na maandishi yakitembea huku na huko katika tovuti mbalimbali hasahasa zile za sanaa na kubadilika rangi n.k
     Sasa unaweza kujiuliza hapa, "Mimi nimesomea Graphic Designing na nimefaulu na kupata cheti kizuri tu lakini mbona siwezi kutengeneza kama wenzangu wanavyofanya?” Jibu la hapa ni rahisi sana na ni vema ukasoma kwa makini makala hii ili upate ufumbuzi wa tatizo lako.
     Kusomea Graphic Designing haina maana kwamba ndio tayari umeshajua kuwatengenezea watu kile wanachotaka. Hapa unafundishwa jinsi ya kutumia hizi program kwa mbinu mbalimbali na kufundishwa jinsi ya kutumia zana zake (tools) kama vile kufuta, kuandika, kuchora mstari, boksi, duara, kujaza rangi, upangiliaji mzuri wa rangi, kukuza unene wa mstari na staili tofauti za maumbo, kupangilia kazi yango vizuri katika utengenezaji, kupimia ukubwa wa document yako kama vile A4, A5, B4 na mengi tu zaidi ya hayo niliyoyataja. Na ndio hayo hayo unayofanyiwa mtihani.        Akili ya ziada zinahitajika ili kuweza kufanya kazi zako kuwa za kuvutia zaidi

comment & share with your friends
Share on Google Plus

About mboo safi nene na ndefu

0 comments:

Post a Comment