Mkanganyiko mkubwa unatokea pale tunapotaka kuchagua kati ya aina hizi mbili za mifumo endeshi kutoka Windows 32-Bit au 64-Bit kwa sababu wengi wetu hatujua nini hasa tofauti zao. Baada ya kusoma makala utafahamu na utachagua chaguo sahihi kwa ajili ya kompyuta yako.
Mfumo endeshi wa Microsoft Windows unakuja katika matoleo tofauti tofauti na kila moja likiwa na kitu cha ziada zaidi ya mwenzi wake, na muda mwingine inakuwa ngumu sana kuona tofauti hizi. Mfano mzuri ni huu wa aina hizi mbili za Windows kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS inakuwa ngumu sana kwa mtumiaji wa kawaida kufahamu tofauti zake.
Microsoft walianza kuachia toleo la 64-Bit katika mfumo wao endeshi uliopendwa zaidi duniani na uliohudumu kwa zaidi ya miaka 14 Windows XP. Kwa mara ya kwanza 64-Bit ilianza kutumika katika mifumo endeshi na kampuni ya Cray mwaka 1985 ikiwa na mfumo endeshi unaofanana kabisa na UNIX – UNICOS. Baada ya hapo aina hiyo ya mifumo endeshi ilitapakaa katika Windows, Mac OS X, Solaris pamoja na Android kwa sasa.
Mifumo endeshi hii ya 32-Bit na 64-Bit inatengenezwa ili kuendana na aina ya Processor inayopatikana katika kompyuta husika, kwa maana hiyo inategemea na aina gani ya processor unatumia ili kuweza kutumia mifumo hii. 32-Bit Windows ilitengenezwa ili kuendana na 32-Bit Processor na 64-Bit hivyo hivyo ili kuendana na 64-Bit Processor. Kwa hiyo kabla y kufanya chochote ni muhimu kufahamu tofauti kati ya aina hizi mbili za processor.
Fahamu ‘bit’ ni nini
Sehumu ndogo kabisa ya data katika kompyuta hufahamika kama ‘bit’ au kwa kirefu ‘binary digit’. Inafahamika kuwa kompyuta inaelewa lugha ya binary tu (lugha ya uwili) yaani ya 0 na 1 kwa hiyo kila bit inaweza ikawa na thamani ya 0 au 1. Kwa hiyo kompyuta huwa inahifadhi data katika makundi ya bit nane nane yanafahamika kama Byte au Octet, na makundi haya kadri yanavyozidi kuwa makubwa ndipo tunapopata Kilobyte, Megabyte, Gigabyte pamoja na Telabyte.
Fahamu Processor ni nini
Processor au CPU ndio ubongo wa kompyuta, kwa maana nyingine processor ndio inafanya kila kitu katika kompyuta kuanzia kupiga ziki, kuangalia picha, kuvinjari katika mtandao pamoja na kazi zote za kompyuta kwa kutumia mahesabu ya 0 na 1 kama tulivyoona katika bit. Wengine huwa wanachanganya CPU na lile jumba linalobeba kompyuta (Computer case).
Ndani ya processor kuna vitu vinavyoitwa Regista na Logical sakiti, sasa hizi regista ndizo zinazosaidia katika kutunza data za ndani ya processor wakati processor ikiendelea na mahesabu ili kufanya shughuli fulani ya kompyuta. Kwa hiyo kuna ukubwa wa regista katika mfumo wa processor wa 32-bit ni 32-bit na hivyo kwa 64-bit ni 64-bit. Kwa hiyo kinachofanya tupate aina hizi mbili za processor ni Regista zilizomo ndani yake.
Kwa hiyo unaona kabisa 64-bit processor inaipa uwezo kompyuta wa kufanya mambo makubwa kwa sababu ina hifadhi kubwa katika ubongo wake (CPU) ukilinganisha na 32-bit processor.
Tofauti kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS
Mifumo endeshi ya Windows yenye 64-Bit ilitengenezwa ili kusapoti kiwango kikubwa cha RAM ukilinganisha na ile ya 32-Bit. Software kubwa kama Autocard, Photoshop, Cinema 4D pamoja na Magemu yanahitaji kiwango kikubwa cha cha RAM hasa inayotolewa na mfumo endeshi mpaka kufikia 16 exabytes. Kiwango cha RAM za kupachika kinachohitajika hutegemea sana na aina ya motherboard unayotumia.
Kiwango kidogo cha RAM kinachohitajika ili mfumo wa 32-Bit ufanye kazi vizuri ni 1GB wakati ule wa 64-Bit unahitaji 2GB na kuendelea. Hii ipo wazi kwani 64-Bit ina regista kubwa hivyo kiwango kikubwa cha RAM kitahitajika. Kama unahitaji kupata matokeo mazuri kutoka kwenye kompyuta ya 64-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 4GB na kuendelea na kwa wale wa 32-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 2GB na kuendelea.
Kitu cha msingi unachotakiwa kufahamu ni kwamba 32-Bit Processor inafanya kazi vizuri tu katika kompyuta ya 64-Bit processor ila hautofurahia uzuri wa processor hii. Unachotakiwa kufanya ni kuweka 64-bit OS. Pia software na Drivers zinahitajika kuwa za 64-bit ili kupata kasi nzuri.
Tatizo kubwa la 64-Bit OS ni kwamba software nyingi zinagoma kufanya kazi na mifumo endeshi hii kwa sababu bado madeveloper hawajatengeneza software za kutosha katika soko zinazoendana na mfumo huu, lakini usihofu kwa sasa utapata software zote za muhimu za 64-bit, mfano Mozila Firefox wameanza kutengeneza kiinjari cha 64-bit hapo Desemba mwaka jana.
Kwa ushauri, kama unaenda kununua kompyuta kwa sasa ni bora ukanunua ya 64-Bit ili kuendana na mazingira ya teknolojia yanayobadilika kwa kasi hivi sasa na ili kupata faida zaidi ya kile unacholipia.
0 comments:
Post a Comment