Taarifa kutoka katika mtandao wa SamMobile ambao unajihusisha na habari zinazohusiana na vifaa na huduma kutoka katika kampuni ya kutengeneza vifaa vya umeme ya Samsung zinasema matoleo ya simu za Samsung Galaxy zinaweza kuanza kupokea maboresho ya Android Nougat hivi punde.
Japo taarifa hiyo haijataja siku au saa ambayo simu hizo zitaanza kupokea maboresho ya mfumo huu kutoka katika kampuni ya Android inayomilikiwa na Google.Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa toleo la maboresho la mfumu huu endeshi kutoka Google lingeanza kupatikana katika miezi ya mwanzo ya mwaka 2017.
Kwa sasa tayari Samsung wametoa toleo la majaribio la mfumu huu endeshi katika simu za Samsung Galaxy S7 na S7 Edge na majaribio haya yanatarajiwa kufikia kikomo katika ya mwezi Desemba mwaka 2016.
Hii inamaanisha matoleo yote ya A series yatapokea maboresho hayo kama Samsung Galaxy A3, Galaxy A5, Galaxy A7, Galaxy A8, Galaxy A9 and Galaxy A9 Pro.
0 comments:
Post a Comment