Top 5 ya simu kali zaidi sokoni kwa mwaka 2017

Tukiwa tumefikia ukingoni kabisa mwa mwaka 2016, swahilitech tumeona tukuletee orodha ya simu kali zaidi zilizobamba na zinazoendelea kubamba sokoni kwa sasa kutoka makumpuni makubwa ya utengenezaji simu.
Mwaka ulianza kwa kampuni ya Samsung kulikamata soko kwa kasi ya ajabu na simu zake za Samsung Galaxy S7 na S7 Edge, huku kampuni ya kichina ya OnePlus nayo ikaja kwa kasi na na simu yake ya OnePlus 3. Moto inayomilikiwa na Lenovo kwa sasa ikatoa Moto Z huku Apple akimalizia mwaka kwa kutoa iPhone 7 S na bila kuisahau Google Pixel.

Hizi hapa simu kali zaidi zilizotoka mwaka 2017

1.  Apple iPhone 7 Plus

Baada ya kuangushwa na Samsung Galaxy S7 Edge katika robo ya kwanza ya mwaka, kampuni ya kimarekani ya Apple iliachia toleo lake la iPhone 7 Plus lililoonekana kufanya vizuri sokoni. Ikiwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha na kutunza chaji, i Phone 7 Plus imeibuka nambari moja katika orodha yetu.

2. Samsung Galaxy S7 Edge

Simu hii kutoka kampuni ya kikorea naweza sema ndio simu bora zaidi ya mfumo endeshi wa Android kutoka katika mwaka 2016. Ikiwa na umbo jembamba lisilokuwa na pembe katika ncha za kioo(edges), simu hii ina kila kitu mtumiaji wa simu alichokihitaji katika karne hii. Samsung walitumia gharama kubwa sana kuitangaza simu hii kabla ya kuitoa.

3. Google Pixel XL

Ukiwa umechoshwa na Flagship za Samsung na Apple, usihofu kuna Google Pixel XL kutoka kampuni ya Google. Simu hii imetoka ikiwa kama mbadala wa iPhone au Samsung kwa wale watumiaji nguli wa simu za smartphones za daraja la juu kabisa. Ukinunua simu hii unapata unlimited storage ya picha katika google photo.

4. Moto Z

Ukitaka simu yenye muonekano mzuri na inayoshikika kiganjani kwa urahisi zaidi, moto Z ndio mahala pake. Kampuni ya Moto iliyochini ya Lenovo imeletea simu ya kwanza ya vipande vipande (modular phone) katika toleo hili la moto Z.

5. OnePlus 3

Kama una kiasi kidogo cha pesa na bado unahitaji simu ya kijanja zaidi, OnePlus 3 kutoka kampuni ya kichina ya OnePlus ndio simu sahihi zaidi kwa mwaka 2016. Na kama OnePlus 3 haitakutosha kwa ukubwa wake wa kioo, usitie shaka kuna OnePlus 3T.
Share on Google Plus

About mboo safi nene na ndefu

0 comments:

Post a Comment