JE RWANDA WANAWEZA KUTUSAIDIA "KITEKNOLOJIA?"



By Malisa GJ,

Kuna vingine ukivisikiliza kama una akili unaishia kucheka na kupuuza. Eti Rwanda itatusaidia wataalamu wa kufufua shirika letu la Air Tanzania, na kwamba Rwanda italeta jopo la wataalamu wa teknolojia ili tuweze kujifunza kwao. Yani Tanzania ijifunze "technology" Rwanda. Hahahah.!

Binafsi naipongeza Rwanda inavyojitahidi kupiga hatua za maendeleo kwa kasi tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994. Imeweza "kurecorver" ktk kipindi kifupi na kuzipiku nchi nyingi za Afrika kwa maendeleo ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha sarafu yake. Hili ni jambo la kupongezwa.

Lakini kusema Rwanda inakuja kutusaidia kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ni kichekesho kikubwa kuliko "comedy za Mr.Bean". Inakuja kusaidia nini kwa mfano?

Wataalamu wa kwanza wa TEKNOHAMA nchini Rwanda (hao ambao serikali ya CCM inawasifia) ni zao la mwaka 2001. Sijui kama unanielewa? Ni hivi; Rwanda kwa mara ya kwanza imezalisha wataalamu wa TEKNOHAMA kutoka nchini humo mwaka 2001. Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Rwanda ilianzishwa mwaka 1997, na ikaanza kuzalisha wataalamu miaka minne baadae.

Wakati Idara hiyo inaanzishwa mwaka 1997, Tanzania ilikua imeshazalisha maelfu ya wataalamu wa TEKNOHAMA wengi wakifanya kazi katika taasisi mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na vyuo vingine vya daraja la kati kama DIT, Mbeya Tech, na Arusha Tech vilikua vimeshazalisha wataalamu wengi sana wa Sayansi na Teknolojia. Yani wakati tukiwa na Maprofesa kadhaa wa mambo ya sayansi na Technolojia, Rwanda hawakua hata na chuo kimoja chenye hadhi ya VETA kinachofundisha technology. Leo tunaambiwa watakuja kutufundisha. Maajabu.!

Nadhani sisi ndio tunapaswa kuwafundisha wao, maana tuna wataalamu wengi kuliko wao. Tuna vyuo vingi vya sayansi kuliko wao, tuna "facilities" na "institutes" nyingi zaidi za technology kuliko wao. Hata Chuo kukuu cha sayansi na Technolojia cha Nelson Mandela kinachotegemewa na nchi zote za SADC kipo Arusha, Tanzania. Sasa Rwanda wanakuja kutufunza nini?

Hata aliyekua Mkuu wa chuo cha Teknolojia Rwanda (KIST), Professor Silas Lwakabamba inadaiwa ni mtanzania na amesoma Chuo Kikuu cha Dar (UDSM), kabla ya kuhamia Rwanda. Baadae Rais Kagame akampa Uraia wa Rwanda na akamteua kuwa waziri wa sayansi na teknolojia.

Wakati Tanzania inaanzisha Shirika la Ndege (Air Tanzania) mwaka 1977, Rwanda walikua wakipanda mabasi, na "matoroli". Walikua wakiona muujiza ndege zetu zikiruka kwenye ardhi yao zimeandikwa "Air Tanzania".

Iliwachukua miaka 25 kuanzisha Shirika lao la "Rwandan Air" (mwaka 2002).

Lakini kwa sasa Rwandan Air ina ndege 16 zinazoruka mataifa mbalimbali duniani, while Air Tanzania ina ndege moja mbovu isiyoweza hata kuruka kutoka "Mabibo hostel" hadi "Pugu Kajiungeni."

Ukweli ni kwamba tuliwatangulia Rwanda ktk maendeleo ya Sayansi na teknolojia lakini kwa sasa wametuacha nyuma. So ni vizuri kuangalia tumejikwaa wapi. Je, tatizo ni wataalamu? Ni fedha? Ni utaalamu au kitu kingine? Kujua chanzo cha tatizo kutasaidia kutafuta "solution" ya kudumu. Lakini tukijidanganya kwenye chanzo cha tatizo hata "solution" tutakayopata itatudanganya, na tutashindwa kuondokana na tatizo.

#Je_Tatizo_Ni_Teknolojia?

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa teknolojia ktk mambo mbalimbali. Hata ktk usafiri wa anga Tanzania ndio yenye "Radar" ya kisasa kuliko nchi nyingine za EAC.

Lakini hata kama shida ingekua technology bado isingekua tatizo kubwa kwa sababu teknolojia inanunulika. Tunaweza kununua teknolojia China, Israel, Marekani etc na tukaiadopt. Inategemea tunakaka technology ya nini.

#Je_Tatizo_ni_Wataalamu?
Tanzania ina wataalamu wengi sana wa masuala ya Sayansi na Teknolojia. However wataalamu wanaweza kutengenezwa. Tunaweza kuchukua raia wetu tukawapeleka nje ya nchi kujifunza na utaalamu watakaoupata wakaja kuutumia kuisaidia nchi.

#SWALI
Ikiwa tatizo si wataalamu, si fedha wala si technology je tatizo ni nini?

#JIBU
Tatizo letu kubwa ni utashi wa kisiasa (Political will). Bado hatujapata viongozi wenye utashi (nia ya dhati) ya kutaka kuiona Tanzania ikipiga hatua ktk sekta ya sayansi na teknolijia.

Either hatuna viongozi wenye utashi wa kisiasa, au wana utashi lakini hawajui njia gani watumie.

Nitakupa mifano michache. Mwaka 2013 kijana mmoja mkoani Arusha alitengeneza Helkopta kwa kutumia Injini ya pikipiki. Helkopta hiyo ilikua na uwezo wa kuruka mita 200 angani na kutua. Hakuna juhudi zozote zilizotumika kumuendeleza kijana huyu.

Mwaka 2014 kijana mwingine mkoani Geita baada ya kuhitimu kidato cha 4 aliweza kutengeneza mfumo wake wa masafa (waves) ambapo watu waliokua mita 500 waliweza "kumsearch" na kumpata kupitia radio zao. Kijana huyu hajulikali alipo kwa sasa.

Mwaka 2008 mmoja wa vijana walioingia "top ten" kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha sita, akipata daraja la kwanza (points 3) mchepuo wa PCM, (jina nalihifadhi) kwa sasa anafanya biashara ya kununua na kuuza magari (chakavu). Licha ya ufaulu mzuri aliopata lakini serikali haikua na mpango wowote wa kumuendeleza ili aweze kuisaidia nchi baadae. Akaenda chuo kikuu kusomea "uhandisi" akamaliza akakaa mtaani bila kazi kwa muda mrefu, saivi kaamua kupiga "deiwaka" ya magari. Ananunua gari anakaa nalo anauza kwa bei ya juu kidogo (apate hela ya kula) ananunua jingine.

Haya ndio maisha ya mtu aliyepata alama "A" masomo yote kidato cha sita. Wakati Israel mtu kama huyu angekua ameendelezwa na serikali na kwa sasa angekua anatumika kwenye idara nyeti, lakini hapa kwetu tumeruhusu auze magari chakavu. Halafu bado tunadhani shida ya nchi yetu ni technology. Huu ni uzwazwa.

Bado hatujajua thamani ya wataalamu wetu. Hakuna utashi wa kisiasa wa kuwafanya wataalamu wetu kuwa "productive and potential" kwa nchi.

#Kwanini_Rwanda_wanafurahia_kutusaidia?

Rwanda wana akili sana. Wametusoma na wamejua shida yetu si teknolojia wala si wataalamu. Lakini wamekubali ombi la kutusaidia kuleta teknolojia na wataalamu. Kwanini?

#JIBU:
Rwanda wamegundua hatujui shida yetu ni nini. Tuna matatizo lakini hatujui "solution" yake. Tunadhani "solution" ni wataalamu au ni teknolojia. Tunatapatapa. Kwahiyo Rwanda wanaitumia fursa hiyo vzr.

Rwanda wanajua shida yetu si wataalamu wala si teknolojia. Lakini wamekubali kutusaidia kwa sababu wamegundua hatujui tatizo letu ni nini. Hivi kama kweli shida yetu ingekua technology tungeacha kwenda kutafuta technology China, Urusi, Marekani, Israel tukatafute Rwanda? Kwa technology ipi ya kina "Ndaizeye"?

So wanyarwanda wameshajua kwamba "hatujielewi" kwahiyo wanaweza tumia fursa hiyo kutuletea wataalamu wa kutufundisha technology "butu", wakati huo wakitumia fursa hiyo kupeleleza mambo mengine yatakayowanufaisha.

Maana yake ni kwamba "wataalamu wa Rwanda" watakuja lakini hatutaona changes zozote kwenye "technology" kwa sababu shida yetu si wataalamu. Tukija kushtutuka na kujua shida yetu, Rwanda watakua washatufaidi vya kutosha.

Ikumbukwe hata Rwanda shida yao haikua "technology" wala wataalamu. Shida ilikua "political will". Utashi wa kisiasa wenye nia ya dhati ya mabadikiko. Hatimaye wakampata Kagame mwenye utashi wa kisiasa, ambaye amewasaidia sana kukua kiuchumi.

Lakini Rwanda hata wangeleta wataalam wote wa teknolojia wa chuo kikuu cha "Havard" bado wasingepiga hatua yoyote kama wangekosa mtu mwenye "good political wiil" (utashi wa kisiasa).

Kwa hiyo Tanzania ili iweze kupiga hatua kiteknolojia na sekta nyingine hatuhitaji kuleta wataalamu kutoka Rwanda wala Congo DRC. Tunahitaji jambo moja kubwa. Utashi wa kisiasa.

Na utashi wa kisiasa wenye tija ni unaoletwa na mfumo, sio unaoletwa na kiongozi mmoja. Rais Obama aliwahi kusema Afrika haihitaji "watu imara" bali taasisi/mifumo imara." Nchi ikiwa na mfumo imara hata kiongozi akifa mfumo huo utaendelea kufanya kazi. Lakini ikiwa na kiongozi imara bila mfumo imara, siku akitoweka kila kitu kinatoweka. #Tafakari.!

Malisa G.J
Share on Google Plus

About mboo safi nene na ndefu

0 comments:

Post a Comment