Alhamisi ya kwanza ya mwezi May kila mwaka ni siku ya Password (neno la siri) duniani. Mwaka huu imeangukia tarehe 5, siku hii ni siku maalumu duniani ya kuhamasisha matumizi bora ya neno la siri ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mtandao na vifaa vingine.
Haya ni mambo saba ya muhimu wakati wa kutengeneza na kutunza password yako
Kiasi cha herufi kinachoshauriwa ni 8, lakini herufi 14 mpaka 25 ni nzuri zaidi japo baadhi ya huduma zina idadi maalumu ya herufi.
Tumia mchanganyiko wa Herufi Kubwa na Ndogo, Tarakimu na Alama tofauti kama !”denG_eZ29$£mtu, baadhi ya huduma haziwezi kukuruhusu kufanya hivyo ila “PaSsWoRd!43” ni nzuri zaidi “password43.”
Epuka maneno yanayopatikana kwenye kamusi, hata kama utaweka namba mbele yake. Kuna baadhi ya programu huwa zinajaribu kutafuta maneno yote yaliyotunzwa kwenye kamusi. Kama utapenda kutumia maneno ya katika kamusi njia rahisi ni kuweka namba katika ya neno kama “pas123swor456d” na sio “password123456.” Njia nyingine rahisi ni kutumia herufi za kwanza za sentensi fulani ili kukumbuka kirahisi kama “napendelea kunywa pepsi cola baridi sana” password itakuwa “nKpCBS0987”
Badili herufi na tarakimu , kama sehemu ya sifuri tumia O, na sehemu ya S tumia lama ya dola $.
Epuka maneno marahisi kutabiri, kama jina lako, tarehe yako ya kuzaliwa, jina la mtoto wako au eneo unaloishi au namba ya simu kama wengi wafanyavyo, na kama unajisikia kufanya hivyo jitahidi kugeuza hayo maneno kutokea nyuma kwenda mbele.
Usirudie password moja katika akunti nyingine, kwa mfano password unayotumia facebook usiitumie instagram au gmail.
Two Factor Authentication kama inavyofahamika zaidi, hii inasaidia pale unapojaribu kuingia kwenye akaunti tofauti yako kwenye kifaa kipya. Akaunti kama za Google watakutaka kuingiza code watakazokutumia kwenye email au simu.
Sisi kama swahilitech tunaunga mkono harakati hizi za kuimarisha usalama wa taarifa zetu za siri katika huduma tofauti.
0 comments:
Post a Comment