*JINSI YA KUIFANYA COMPUTER YAKO IJIZIME YENYEWE KWA MUDA UNAOUTAKA WEWE
Inawezekana wewe ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakijikuta wanapitiwa na usingzi na kuiacha computer ikiwa on. Au inawezekana huwa unapata shida pale unapotaka kuondoka wakat mtoto /mdogo wako anataka aendelee kuangalia katuni au kucheza gem.
Kwa kuzingatia sababu mbalimbali, leo nimeona nifanye somo hili kwaajili yako. Kifupi ni kwamba unaweza kuiamrisha computer yako izime kwa muda unaoutaka wewe kwa kufata hatua hizi rahisi.
HATUA
1. a) bonyeza windows button (hii ni button yenye alama ya nembo ya windows) na R kwa pamoja. Itatokea sehem ya kusearch(sehem hiyo huitwa RUN) andika CMD (hiki ni kifupi cha neno Command prompt) then bonyeza ENTER
b) ukishindwa nenda kwenye sehem ya kusearch na uandike RUN utaiona then ibonyeze halaf andika CMD then ENTER
C) Ukishindwa nenda sehem ya kusearch andika CMD then ibonyeze.
2. Kitatokea kipage cheusi chenye maandishi meupe
Andika shutdown -s -t then weka muda unaoutaka. Kumbuka muda huwa unakuwa kwa sekunde kwahiyo kama unataka kuset ijizime baada ya dakika moja utaandika shutdown -s -t 60 then bonyeza ENTER.
3. Computer yako itakuletea ujumbe ikikwambia kwamba computer yako itajizima baada ya dakika 1. (Hiyo itategemeana na muda uliochagua wewe)
Naamini nimeeleweka.unaweza kujaribu mwenyewemwenyewe
*****Thanks endelea kutembelea blog hii kila siku upate maarifa****
0 comments:
Post a Comment